Wednesday, April 6, 2011

JAMANI MBAGALA!!




Hapa ni maunganikio ya barabara ya Kilwa iliyojengwa na Kajima na ile ya zamani kuelekea mikoa ya kusini, panaitwa Mbagala Rangitatu. Ninatumia sana njia hii kwa safari zangu za Dar es Salaam kwenda Mtwara. Ukiwa unatokea kusini, sehemu hii inakera! Waweza tumia mmasaa mawili hadi matatu kabla ya kuvuka hapa, ni pabovu kuliko Somanga - Ndundu. Kuna halmashauri ya Manispaa ya Temeke pamoja na Mbunge wa kigamboni nyote mnatukera! Mnakera kwa sababu nyie ni wababaishaji, kipande cha meta 100 hakiwezi kukwamisha watu kwa masaa mengi namna hii. Hebu fikiria wewe ni askari wa usalama barabarani na hapo unatakiwa uongoze magari, unatakiwa kuvaa unifomu gani? Mnakera!

No comments:

Post a Comment