Tuesday, July 13, 2010

UJENZI WA BARABARA SHANGANI - MTWARA




Hili ni bango la Mkandarasi wa barabara kule Shangani west - Mtwara. Kwa wenyeji, limewekwa hapo muda mrefu (zaidi ya miezi 6) bila ujenzi wowote kuendelea. Hapa nimelikuta likiwa limeanguka chini , wasamalia walilisimamisha ili niweze kupata taswira nzuri! Ujenzi huu ulisababisha kufungwa kwa kituo cha daladala cha Kambarage, sijui watumiaji wa kituo hiki imewagharimu kiasi gani kwa muda wote ili kufikia kilipo kituo kipya? TAFAKARI!!

No comments:

Post a Comment